RAIS MAGUFULI AZITAKA MAHAKAMA ZITENDE HAKI....."NI AIBU NCHI KUWA NA MAHABUSU WENGI KULIKO WAFUNGWA"


Rais  Magufuli amezitaka mahakama nchini kutenda haki kwa kuhakikisha watu waliopo mahabusu wanastahili kuwa huko kwani wengi wao wanakuwa hawana makosa hali inayosababisha kuwa na mahabusu wengi kuliko wafungwa jambo linaloiletea nchi aibu.Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 18, alipokuwa akizindua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato mkoani Geita na kuweka jiwe la msingi wa ujenzi Jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

“Nikuombe Jaji Mkuu na Jaji kiongozi muendelee kulisiamamia jambo hili la mahabusu lakini niviombe vyombo vingine vya utoaji haki, polisi wanaohusika kupeleleza na ofisi ya mwanasheria mkuu hakikisheni watu waliopo mahusu ni wale wanaostahili kuwepo huko kwani ni aibu kuwa na wafungwa wachache kuliko mahabusu.

“Kuwa na mahabusu wengi katika magerezani yetu sio sababu ya mahakimu au majaji sababu kubwa ni kwa hawa wengine ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao, nchi hii sio ya kukaa na mahabusu tu wanalia kule wakati wengine hawana makosa na ninalizungumza hili kwa majonzi makubwa sana.

“Zaidi ya nusu ya watu waliopo magerezani ni mahabusu wanaosubiri kusikilizwa kwa kesi zao kabla ya msamaha nilioutoa magereza yetu yalikuwa na watu 35,803 ambapo wafungwa walikuwa 17,547 na mahabusu walikuwa 18,256 hivyo basi nina imani kuwa ujenzi wa mahaka utasaidia kupunguza tatizo hilo la mahabusu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha amelipongeza Jeshi na Zimamoto na Uokoaji kwa kukusanya takribani Sh bilioni 73,264 katika kipindi cha miaka mine iliyopita ambapo amesema kuwa hii inaonesha wazi kuwa kazi yai sio kuzima moto tu au kushugulikia majanga bali wanakusanya pia mapato kwaajili ya serikali na mapato hayo ndio yanaenda kutumika kwenye huduma mbalimbali.

“Ninatambua kuwa kwa baadhi ya watu ukitoa pongezi kwa jeshi la zimamoto ni lazima watashangaa kwasababu kati ya taasisi zinazolaumiwa na wananchi kwa utendaji usioridhisha ni pamoja na jeshi hili japokuwa ninajua wakati mwingine wanalaumiwa kwa makosa yasiyokuwa yao, utakuta wakati mwingine wanalaumiwa kumbe tatizo ni taarifa kuchelewa kuwafikia au kutokana na ugumu wa kufika kwenye eneo husika kutokana na watu wengine kujenga kiholela lakini sina budi kuwapongeza kwa kazi kuwa wanazozifanya, mnyonye mnyongeni haki yake mpeni,” amesema Rais Magufuli.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post