PAPA MSOFE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UTAKATISHAJI FEDHA, UHUJUMU UCHUMI


Mfanyabiashara maarufu Marijan Msofe maarufu ‘Papaa Msofe’ na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo utakatishaji wa fedha wa zaidi ya TSh.Mil 900.


Mbali na Msofe, washitakiwa wengine ni Wakili wa Kujitegemea, Mwesigwa Mhingo,Fadhil Mganga, Wencelaus Mtui na Joseph Haule na miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni Kuratibu Genge la uhalifu,utakatishaji fedha na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili mwandamizi wa Serikali Ladslaus Komanya amedai washtakiwa wanadaiwa kufanya makosa hayo kati ya Desemba 2018 na Septemba 2019 ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambapo walijipatia zaidi ya Shilingi Milioni 900.
 

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi, hivyo haina dhamana ambapo shauri hilo limehairishwa hadi December 16, 2019.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527