MUUGUZI ADAIWA KUBAKA MAMA MJAMZITO AKIWA CHUMBA CHA KUJIFUNGULIA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia ofisa muuguzi msaidizi wa kituo cha afya Mamba Wilaya ya Mlele, Abednego Nkona (32) kwa tuhuma za kumbaka mjamzito wakati akijifungua.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga  alisema tukio hilo la kinyama na la kikatili  lilitokea Desemba  18, mwaka huu saa 2 usiku katika chumba cha kujifungulia wajawazito.

 Alisema siku ya tukio, mwanamke huyo  alipatwa na uchungu wa kujifungua baada ya siku zake kutimia, alitoka nyumbani kwake Majimoto  kwenda kupata huduma kituoni hapo, huku akisindikizwa na mama yake mzazi.

Baada ya kufika kituoni alipokelewa na Alfred ambaye alikuwa muuguzi wa zamu siku hiyo.

Alisema muuguzi alianza kumpatia huduma ya uzazi, lakini mwathirika wa tukio hilo alihisi  hali isiyo ya kawaida  sehemu zake za siri  hali ambayo ilimfanya ashituke.

Alisema  baada ya kubaini hilo na kuingiliwa licha ya kuwa hatua za mwisho kujifungua alipiga kelele.

Alisema baada  kuona hivyo,  mjamzito aliamua  kuinuka  kitandani  na kwenda  moja kwa moja  kutoa taarifa  kwa  mama yake mzazi, Mektilida  Deogratius  ambaye alitoa taarifa kwa uongozi wa kituo.

Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho, alitokomea kusikojulikana, lakini polisi  walifanikiwa kumkamata.

 Kamanda Kuzaga, alisema  mtuhumiwa   anaendelea kushikiliwa na anatarajiwa  kufikishwa mahakamani  wakati wowote  ili akajibu  tuhuma hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527