SERIKALI YAZINDUA MRADI WA UJENZI DIT MWANZA, KUGHARIMU TSH. BILIONI 37 | MALUNDE 1 BLOG

Friday, December 20, 2019

SERIKALI YAZINDUA MRADI WA UJENZI DIT MWANZA, KUGHARIMU TSH. BILIONI 37

  Malunde       Friday, December 20, 2019


Serikali imezindua mradi wa ujenzi wa majengo mapya ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kampasi ya Mwanza wenye thamani ya Sh. Bilioni 37 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (World Bank).

Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha sambamba na mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo katika kampasi ya Mwanza ambapo amesema ujenzi huo utaanza karibuni na unatarajiwa kukamilika Desemba 2024.

Ole Nasha ameongeza kuwa mradi huo utaongeza udahili kwa zaidi ya asilimia 50 katika fani mbalimbali za ufundi na teknolojia na utawezesha kuhuisha mitaala katika fani ya ngozi ili kuzalisha mafundi mahiri watakaoweza kujiajiri na kuajiriwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post