Picha : TRA YATOA ELIMU YA KODI KWA WAANDISHI WA HABARI MANISPAA YA SHINYANGA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendesha semina ya Elimu ya Kodi,matumizi ya mashine za EFD na mfumo wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa Waandishi wa Habari waliopo katika Manispaa ya Shinyanga.


Semina hiyo ya siku moja imefanyika leo Ijumaa Desemba 20,2019 katika ukumbi wa TRA mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa Magazeti,Redio, Televisheni na Mitandao ya Kijamii.

Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Anthony Faustine amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuhusu masuala a Kodi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT).

"Tumekutana na waandishi wa habari kwani tunaamini kuwa waandishi wa habari ni wadau muhimu wakielewa vizuri kuhusu masuala ya kodi watasaidia pia kuielimisha jamii hivyo elimu hii itawafikia Watanzania wengi zaidi",amesema Faustine.
Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Anthony Faustine akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari Manispaa ya Shinyanga kuhusu masuala ya Kodi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Anthony Faustine akitoa elimu ya kodi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT) kwa waandishi wa habari wa Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Anthony Faustine akitoa elimu ya kodi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT) kwa waandishi wa habari wa Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Anthony Faustine akitoa elimu ya odi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT) kwa waandishi wa habari wa Manispaa ya Shinyanga.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakifuatilia mada ukumbini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post