MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA KUANZIA KESHO JUMAMOSI


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wakazi wa mikoa 15 nchini kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa inayotarajia kunyesha.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Ijumaa Desemba 20, 2019 imeitaja mikoa hiyo ambayo mvua hizo zinatarajia kunyesha kesho Jumamosi ni; Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Zanzibar.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post