MAALIM SEIF AWAPONZA" MAKAMANDA WA POLISI.....NAIBU WAZIRI MASAUNI AAGIZA WAONDOLEWE


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Simon Sirro kuwaondoa Makamanda wa Polisi wa Mikoa Miwili ya Kusini Pemba   na Kaskazini Pemba kwa kushindwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 16 za Makazi ya Polisi uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018 na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan pamoja na kuacha mikutano ya siasa ya Chama cha ACT Wazalendo  kuendelea Kisiwani Pemba  hali ambayo  kukaidi agizo la Kiongozi Mkuu wa Nchi.


Masauni ametoa agizo hilo jana Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.

Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na  Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527