LAZARO NYALANDU ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA KATI

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kati kwa kupata kura 60 kati ya 86 zilizopigwa na kumshinda aliyekuwa mwenyekiti wa kanda hiyo, Alphonce Mbasa.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumapili Desemba Mosi, 2019, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick Sosopi akisaidiana na katibu mkuu wa baraza hilo, Julius Mwita. amesema waliopiga kura walikuwa 86, hakuna kura iliyoharibika.


Amesema aliyekuwa mwenyekiti wa Kanda hiyo, Alphonce Mbasa amepata kura 26, sawa na asilimia 33.2.

Katika nafasi ya mweka hazina, Mbunge wa Viti Maalum,  Devotha Minja ameibuka mshindi baada ya kupata kura 44 sawa na asilimia 51.2 huku mshindani wake, Tully Kiwanga akipata kura 42 sawa na asilimia 48.8.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post