IGP SIRRO ASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUWAJENGEA UWEZO MAOFISA NA ASKARI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, December 21, 2019

IGP SIRRO ASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUWAJENGEA UWEZO MAOFISA NA ASKARI

  Malunde       Saturday, December 21, 2019

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitano utakaosaidia katika kuwajengea uwezo maofisa na askari wa Jeshi hilo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Akisaini mkataba huo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma IGP Sirro amesema kuwa, wameendelea kushirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba  Mwekundu ICRC katika kuhakikisha wanaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa maofisa na askari kuhusiana na masuala ya haki za binadamu.

Kwa upande wake Mkuu wa Misheni Andrea Heath amesema kuwa, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC imeendelea kuwa na ushirikiano mzuri na Jeshi la Polisi nchini na kwamba mkataba huo wa miaka mitano utasaidia katika kufanya mafunzo mbalimbali ikiwemo semina za masuala ya baharini huku lengo likiwa ni kupunguza uhalifu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post