HAKIMU AMTAKA TUNDU LISSU AFIKE MAHAKAMANI KESI YA UCHOCHEZI

Mahakama ya Kisutu imesisitiza kuwa inamtaka Mahakamani aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi.

Hata hivyo, Lissu ameieleza Mahakama kupitia Mdhamini wake Ibrahim Ahmed kuwa anahitaji kurejea ila bado anahofia usalama wake, kesi imeahirishwa hadi Januari 20,2020. 

Novemba 21, 2019 Mahakama hiyo iliwataka wadhamini wa mwanasheria mkuu huyo wa Chadema kuhakikisha wanampeleka mahakamani ili kesi ya msingi iendelee.

Katika maelezo yake mahakamani, Ahmed amedai alifanya utaratibu kama alivyoelezwa na Mahakama, alipomfikishia mteja wake agizo hilo alijibiwa kuwa anatamani kurejea nchini lakini ana hofu na usalama wake.

Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto amedai upande wa mashtaka umeshindwa kuleta mashahidi kutokana na mshtakiwa wa nne kutokuwepo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alimsisitiza mdhamini huyo kuhakikisha Lissu anafika mahakamani kwa kuwa taratibu za dhamana zinaeleweka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 20, 2020.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post