MKUU WA MKOA WA KAGERA AMESEMA HATAKI KUSIKIA SUALA LA UPUNGUFU WA MADARASA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali  Marco Gaguti
Na Ashura Jumapili - Malunde 1 blog
MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali  Marco Gaguti,amesema  hataki kusikia suala la upungufu  wa madarasa na kuzitaka halmashauri zote za Wilaya mkoani humo kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapokelewa na kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020.

Brigedia Jen.Gaguti,alitoa agizo hilo katika kikao cha wadau wa elimu mkoani humo kilichofanyika katika Manispaa ya Bukoba.
“Wanafunzi wote waliofaulu wapokelewe kwenye shule walizopangiwa  kwa wakati kwaajili ya kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza”alisema BrigediaJen.Gaguti.
Awali Ofisa elimu mkoa wa Kagera Juma Mhina,alisema kuwa mkoa wa Kagera una kabiliwa na upungu wa vyumba vya madarasa 283.
Mhina ,alisema halmashauri zinahimizwa kushirikisha jamii na wadau mbalimbali wa elimu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati ili ifikapo mwezi Machi ,2020 wanafunzi waliofaulu waweze kujiunga na kidato cha kwanza.
Alisema Wilaya inayoongoza kwa upungufu wa vyumba vya madarasa ni Wilaya ya Muleba vyumba 66,Karagwe vyumba 56,Biharamulo vyumba 37,Kyerwa 32,Bukoba Manispaa 32,halmashauri ya Bukoba 32,Missenyi 31 na Ngara vyumba 8.

Mwalimu Aidan Bahama,ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ngara ,alisema jitihada za kupunguza  uhaba  wa vyumba vya  madarasa zilizotokana na  kikao cha wadau wa elimu cha mwaka 2018 wilayani humo.
Bahama,alisema Wilaya ya Ngara mwaka jana ilikuwa na upungufu  wa vyumba saba vya madarasa .
“Tuliona kuna upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa  kwa shule za sekondari na msingi ,Wilaya ilifanya tathimin  kuona shule zenye upungufu  na idadi ya madarasa yanayohitajika kwa shule husika”alisema mkurugenzi.
Alisema baada ya tathimini  mkurugenzi na mkuu wa Wilaya ya Ngara walishirikiana  wakaamua  kujenga vyumba  Zaidi ya vilivyokuwa vinahitajika hivyo walijenga vyumba 22 badala ya vyumba 7.

Alisema Rais kupitia kwa Wazairi wa Tamisemi alitoa kiasi cha shilingi milioni 25 kwa kila shule ambazo zilisaidia kukamilisha maboma  yaliyokuwa hayajakamilika na kuongeza vyumba vingine na kuwa na jumla ya vyumba 48 vya madarasa.

Alisema hata huo upungufu wa vyumba vya madarasa 8 mwaka huu vipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji  hadi kufika mwezi Januari 2020 hakutakuwa na upungufu wa chumba hata kimoja.
Alisema mafanikio hayo ni nguvu ya pamoja kati ya mkurugenzi,mkuu wa wilaya,wananchi na wadau wa elimu wilayani ngara.
Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post