DEREVA ATAKAYEPATIKANA NA MAKOSA KUFUTIWA LESENI

Na Amiri Kilagalila-Njombe

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani nchini limesema kuwa litawakamata na kuwafungulia mashataka na kuwafutia leseni madereva na wahudumu wengine katika vyombo vya usafiri watakaokiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo makosa ya mwendokasi na kujaza abiria kupita kiasi  kuelekea msimu sikukuu za krismasi na mwaka mpya.

Jeshi la polisi limeyasema hayo katika oparesheni ya ukaguzi wa mabasi iliyofanyika mjini Makambako mkoani Njombe ikiongozwa na mrakibu wa polisi Abel Swai ambaye ni mkuu wa kitengo cha elimu, mafunzo na uenezi wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani.

“Jeshi la polisi limejipanga vizuri hasa kuelekea hizi sikukuu za mwisho wa mwaka,kwa hiyo wewe ambaye utatujaribu tutapambana na wewe na ndio maana tunasema tunanyakuwa kimya kimya kwa kishindo,tukikumata pingu jela na tunakuacha unatulia kule,lakini tukibaini matendo yako uliyoyafanya hayafanani na matakwa ya sheria tutapurura madaraja yote ya leseni tutakwambia wewe sasa hivi ukafanye shughuli nyingine”alisema Abel Swai

Oparesheni hiyo imefanyika kwa kutoa elimu kwa maafisa usafirishaji na abiria pamoja na madereva akiwemo Godfrey Nkwama ambapo wamesema kitendo hicho cha ukaguzi wa magari wa mara kwa mara ni kizuri ili kupunguza ajari

Hata hivyo mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Njombe Jane Warioba  amesema ajali za barabarani zimekuwa zikipungua kwa asilimia 6 kwa mkoa wa Njombe ndani ya miaka miwili iliyopita.

“Madereva waendeshe kwa tahadhari,lakini pia kwa kipindi cha mwaka 2019 tumepunguza ajari kwa kiasi kikubwa sana kwa asilimia 6 ukilinganisha na mwaka 2018”alisema Jane Warioba


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527