RAIS MAGUFULI: HAKUNA CHAKULA CHA BURE KWA WAVIVU....NENDENI MKALIME ASIYE FANYA KAZI ASILE NA ASIPOKULA AFE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, November 27, 2019

RAIS MAGUFULI: HAKUNA CHAKULA CHA BURE KWA WAVIVU....NENDENI MKALIME ASIYE FANYA KAZI ASILE NA ASIPOKULA AFE

  Malunde       Wednesday, November 27, 2019

Rais Magufuli amesisitiza msimamo wa Serikali wa kutotoa chakula cha msaada kwa wananchi watakaokumbwa na njaa kwa uvivu wa kulima.


Amesema mvua zimeanza kunyesha na majaruba ya mpunga yamejaa maji, hivyo amewataka  watu waende wakalime   na kuchapa kazi kwa bidii  ili kuzalisha chakula cha kutosha.

“Kila mtu afanye kazi. Hata kwenye Biblia imeandikwa asiyefanya kazi na asile na asipokula afe.” Amesema Rais Magufuli leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga

“Mvua zinanyesha za kutosha; naamini majaruba ya mpunga yamejaa maji. Tuna ardhi ya kutosha yenye rutuba; kila mtu alime na kuchapa kazi kwa bidii kuzalisha chakula cha kutosha yeye na familia yake na ziada ya kuuza kwa ajili ya mahitaji mengine,” amesisitiza Rais Magufuli l

Amewashauri Watanzania kuacha kilimo cha mazoea kwa kuendelea kung’ang’ania mazao ya asili ambayo baadhi hayastahimili ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post