RAIS MAGUFULI AVITAKA VYUO VIKUU VIPUNGUZE KUTEGEMEA MISAADA YA NJE KATIKA TAFITI ZAKE


Vyuo vikuu nchini vimetakiwa kufanya tafiti mbalimbali kulingana na mahitaji na vipaumbele vya nchi na kupunguza kutegemea misaada ya nje kwenye tafiti zao kwakuwa wanaotoa misaada ndio wanaowapa ajenda ya utafiti.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Novemba 21, na Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM), baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa katika Sayansi ya chuo hicho.

“Ili kukuza uwezo wa kujitegemea katika gharama za utafiti anzisheni na imarisheni mifuko yenu ya fedha za utafiti, tafuteni njia mbalimbali za kuimarisha mifuko hiyo ikiwemo kutumia taaluma zenu mlizonazo, serikali kwa upande wake itaendelea kusaidia kwa kuongeza mchango wake katika mfuko wa utafiti wa kitaifa nchini ili kwa kushirikiana na jitihada za vyuo vikuu katika kuimarisha uwezo wetu wa ndani wa kugharamia tafiti zetu zinazobeba ajenda zetu wenyewe.

“Tafiti na matokeo ya tafiti hizo zitakuwa na maana tu ikiwa zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wetu, anagalieni namna tafiti zenu zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa, bainisheni matatizo na tafuteni majibu ya yanayowakabili wazalishaji mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji madini na wenye viwanda” amesema Raisi Magufuli.

Ameongeza kuwa ni lazima vyuo vyote nchini viwe chimbuko la maarifa mapya na chahu ya maendelo akidai haitasaidia iwapo matokeo ya tafiti, maarifa, ujuzi na mbinu zinazozalishwa vyuoni havitatumiwa na Watanzania wenyewe ndio maana serikali ya awamu ya tano imejitahidi kutumia wataalamu wa ndani katika kutafuta majibu ya mambo mbalimbali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post