MFUGA NYOKA AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA NYOKA WAKE | MALUNDE 1 BLOG

Monday, November 4, 2019

MFUGA NYOKA AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA NYOKA WAKE

  Malunde       Monday, November 4, 2019
Mwanamke mmoja amekutwa amekufa katika jimbo la Indiana nchini Marekani huku nyoka mwenye sumu akiwa amemzunguka katika shingo.

Laura Hurst ambaye alikuwa na umri wa miaka 36, amekutwa maiti na polisi mara baada ya kufika katika mji wa Oxford.

Nyumba hiyo ilikuwa na nyoka 140 ndani, jambo ambalo inaaminika kuwa nyumba hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi wanyama.

Nyoka wapatao 20 wanamilikiwa na bi Hurst ambaye alikuwa anawatembelea mara mbili kwa wiki.

Ingawa nyumba hiyo inadaiwa kuwa inamilikiwa na mkuu wa polisi katika kaunti ya Benton, Don Munson ambaye anaishi nyumba jirani.

Anasema kuwa alimkuta Hurst kwenye sakafu, gazeti la nchini humo linaripoti.

Aliliambia gazeti hilo kuwa kifo cha bi Hurst kilikuwa ni "ajali kubwa na amekuwa akionyesha ushirikiano na kila mtu".

Kamanda polisi katika jimbo la Indiana, Kim Riley anasema kuwa mtu huyo ambaye alimkuta Hurst aliweza kuwaondoa nyoka hao shingoni lakini watu wa dharura walipofika walishindwa kumuokoa.

Bi.Hurst, alijeruhiwa na nyoka hao ingawa ni kitu ambacho alikuwa anakifanya kila wakati bila kudhurika.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post