MWENYEKITI WA NCCR-MAGEUZI, JAMES MBATIA ASHAURI MUDA WA KUCHUKUA FOMU SERIKALI ZA MITAA UONGEZWE


Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amemtaka Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo kuongeza muda kuchukua fomu za uchaguzi wa Serikali za mitaa kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza.

Wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa walianza kuchukua na kurejesha fomu kuwania uwenyekiti wa kijiji, mtaa, kitongoji na ujumbe wa kamati ya mtaa kuanzia Oktoba 29, 2019. Shughuli hiyo inayofanyika kwa siku saba itakamilika Novemba 4, 2019.

Akizungumza mjini Dodoma jana Jumamosi Novemba 2, 2019 Mbatia alisema baadhi ya maeneo ofisi zilifunguliwa siku mbili tu, baada ya hapo zilifungwa jambo lililowakosesha  nafasi wagombea wengine kuchukua fomu.

Amesema Serikali imetoa muda wa siku saba kwa ajili ya wagombea kuchukua na kurudisha fomu lakini baadhi ya vituo vinafungwa kabla ya muda.

Amesema malalamiko ni mengi kila kona, na kumtaka Jafo kuongeza muda ili wenye nia ya kugombea kujitokeza kwa wingi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527