MBUNGE BALOZI ADADI AISHUKURU SERIKALI KUWASAIDIA KUWEKA LAMI KWENYE MJI WA MUHEZA



MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa halfa ya utiliaji saini  ya kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 kwenye mji huo kwa kiwango cha lami kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Nassib Mbaga na kushoto ni Meneja wa Tarura wilaya hiyo Mhandisi Joseph Kahoza

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Nassib Mbaga akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia ni Katibu  wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo 
 Meneja wa Tarura wilaya hiyo Mhandisi Joseph Kahoza akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akimkabidhi nyaraka na michoro mkandarasi wa kampuni ya ujenzi SIMAC LTD kutoka Dar Felix Chawe mara baada ya kusaini nae mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 katika mji wa Muheza

 MBUNGE wa Jimbo la Muheza kushoto Balozi Adadi Rajabu (aliyevaa suti) akisisitiza jambo kwa mkandarasi wa ujenzi huo mara baada ya kutembelea eneo ambalo ujenzi huo utafanyika 
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akimsikiliza Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo kulia wakati walipotembelea barabara ya sokoni wilayani humo 



MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuwasaidia kuweka lami baadhi ya barabara zilizopo kwenye mji huo. 

Huku akiwataka wananchi wilayani humo kumpa ushirikiano mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi huo ili aweze kutekeleza kazi yake kwa wakati kutokana na kwamba amepewa muda wa miezi saba. 



Balozi Adadi aliyasema hayo wakati wa halfa ya utiaji wa saini kati ya kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 kwenye mji huo. 



Alisema kwamba utiliaji saini huo umeonyesha namna serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha inaboresha miundombinu kwenye miji mbalimbali hapa nchini. 

Mbunge huyo alisema kwamba barabara ni kilomita ya pili ambayo itaanzia Kilimanjaro Bar, Darajani, relini mpaka hospitali ya Teule Muheza na baadae kufika mpaka kwenye kipande ambacho kinatumika na wananchi kwenye maeneo ya karibu na soko la Muheza. 

“Serikali ya awamu ya tano imeweza kutusaidia kuweka lami ni jambo kubwa na la faraja kubwa kwetu hivyo kwa sababu lami itawekwa kwenye mji wetu hakikisheni mnapa ushirikiano na niwaombe msimpe vikwazo vya namna yoyote ile “Alisema Balozi Adadi. 



Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Tarura wilaya ya Muheza Mhandisi Joseph Kahoza alisema kwamba mkandarsi aliyekabidhi mkataba huo ni wa barabara za mita 800 kwa ajili ya kuweka lami kwa mji wa muheza. 

Alisema mkandarasi huyo ataanza kufanya kazi hiyo kuanzia barabara ya Kilimanjaro darajani, relini mpaka teule ambao utakuwa na thamani ya milioni 386 huku akieleza barabara nyengine ya mita 200 zinazokarabatiwa mjini humo zitatumia zaidi ya milioni 60.. 

Naye kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi SIMAC LTD kutoka Dar Felix Chawe ambao wamekabidhiwa barabara hiyo alisema kwamba anajisikia furaha kupata nafasi ya ujenzi huo huku akihitaji ushirikiano na kuhaidia kufanya kazi kwa uwezo wake wote na maelekezo yaliyopo kwenye mkataba. 

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527