MAREKANI YATAKA MAKAMPUNI YA MITANDAO YA KIJAMII KUZIFUTA AKAUNTI ZA VIONGOZI WA SERIKALI YA IRAN | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, November 24, 2019

MAREKANI YATAKA MAKAMPUNI YA MITANDAO YA KIJAMII KUZIFUTA AKAUNTI ZA VIONGOZI WA SERIKALI YA IRAN

  Malunde       Sunday, November 24, 2019
Marekani imeyataka makampuni ya Facebook, Instagram na Twitter kuzifuta akaunti za viongozi wa serikali ya Iran hadi pale nchi hiyo itakaporejesha mtandao wa intaneti nchi nzima. 


Iran imezima intaneti nchi nzima kwa zaidi ya wiki moja katikati mwa ghasia zilizotokana na maandamano. 

Mwakilishi maalum wa Marekani nchini Iran, Brian Hook amesema utawala wa Tehran umejaa unafiki kwasababu wanazima intaneti lakini serikali inaendelea kuitumia mitandao. 

Amesema wameyataka makampuni hayo matatu kuzifunga akaunti za viongozi wa juu akiwemo Ayatollah Khamenei, waziri wa mambo ya nje Zarif Javad na rais Hassan Rouhan, hadi pale watakaporejesha intaneti. 

Maandamano yaliibuka Novemba 15 nchini Iran, saa chache baada ya tangazo la kupanda kwa bei ya mafuta. Siku iliyofuata serikali ilizima intaneti katika hatua ya kuzuia usambazaji wa vidio za maandamano.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post