RADI YAUA WATATU RUKWA


Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, Justine Matejo, amethibitisha kutokea kwa matukio mawili ya vifo ambavyo vimesababishwa kwa mvumo wa radi, hali iliyopelekea watu watatu kufariki Dunia.

RPC Rukwa amesema, wamepokea taarifa hizo za matukio mawili tofauti ambalo moja lilitokea Novemba 23 saa 8:30 mchana, na lingine ni Novemba 19.

"Ni kweli kuna taarifa ambazo tumezipata kwamba huko maeneo ya Namanyele kuna kijiji kinaitwa Mwai, kuna watu wawili wamepigwa radi ambao walikuwa wamejihifadhi chini ya mti, hivyo radi ikapiga mti na watu hao wakapoteza maisha, watu hao ni Japhet Gerrald (25) na mtoto Peter Richard (8)" amesema

"Kuna tukio lingine ambao ni la muda lilitokea Novemba 19, maeneo ya kijiji cha Lahela Mume na Mke ambao walikuwa wamelala, kwa bahati mbaya radi ilipiga ila aliyefariki alikuwa ni Mke" ameongeza

Aidha RPC Rukwa ametoa rai kwa wakazi wa mkoani humo kwa kuchukua tahadhari kuwa wasikae katika miti kwa sababu inakuwa ni tatizo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post