JESHI LA POLISI LAMSAKA MKUFUNZI ALIYESABABISHA MAUAJI YA VIJANA WAWILI WALIOKUWA KWENYE MAFUNZO YA JESHI LA MGAMBO


Polisi Mkoani Singida wanamsaka Mkufunzi Msaidizi wa Jeshi la Akiba Said Ng'imba kwa tuhuma za mauaji ya Vijana wawili waliokuwa kwenye mafunzo ya Jeshi la Mgambo Kata ya Mudida Singida.

Kamanda wa Polisi Singida, Sweetbert Njewike amesema Wanafunzi hao wanadaiwa kufariki baada ya kupewa adhabu iliyopitiliza kwa kutakiwa watumbukie ndani ya dimbwi lililojaa maji ya mvua kitendo kilichopelekea wapoteze maisha kwa kushindwa kupumua.

Inadaiwa Mkufunzi aliwapa adhabu hiyo baada ya Wawili hao kutuhumiwa kutoshiriki ipasavyo mafunzo ya November 19 mwaka huu.

"Wanafunzi hao baada ya kutumbukia kwenye maji hawakuibuka, Mkufunzi akatoweka haraka na kukimbiia kusikojullikana, tunaendelea kumsaka"-Amesema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527