BIBI WA MIAKA 82 AMTEMBEZEA KICHAPO KIJANA WA MIAKA 28


Bibi Willie Murphy wa miaka 82 ambaye alikuwa mtunisha misuli.

Bibi Willie Murphy mwenye umri wa miaka 82, kutokea jijini New York nchini Marekani, amempiga mwanaume wa miaka 28, ambaye jina lake halikuwekwa wazi kwa kosa la kuvamia nyumbani kwake bila ruhusa majira ya saa 5:00 usiku.

Bibi huyo ambaye inadaiwa alikuwa anafanya michezo ya kutunisha misuli 'Bodybuilder' enzi za ujana wake, amesema alikuwa anaenda kulala chumbani kwake, ghafla akasikia mtu anagonga hodi mlangoni huku akidai kutaka kupigia gari la msaada wa wagonjwa lije nyumbani kwake.

Bibi huyo ameendelea kusema jamaa huyo aliamua kuvunja mlango wake na kuingia ndani kwa nguvu na ndipo yeye alipojihami kwa kuwapigia simu polisi, huku ameshika gongo na meza kisha kuanza kumpiga nazo jamaa huyo.

Baada ya polisi kufika Bibi huyo alinukuliwa akisema "Ilikuwa ni usiku na niko pekee yangu, mimi ni mzee, lakini wajua nini, nilichukua meza na gongo nikampiga navyo, Polisi walivyoingia, tayari alikuwa amelala chini kwa sababu nilikuwa nishamaliza kazi" amesema Bibi Willie Murphy.

Willie Murphy aliwahi kuwa mshindi wa mataji kadhaa ya michezo ya kutunisha misuli na anaamini ujasiri alioufanya utawatia moyo watu wenye umri kama wake.

Chanzo cha habari hii ni Tuko News.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post