RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 60 KWA MASHIRIKA NA TAASISI YASIYOTOA GAWIO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 60 , kwa mashirika na taasisi ambazo hazijatoa gawio kwa Serikali, na kuagiza baada ya miezi hiyo miwili kama watakuwa hawajakabidhi gawio kwa Waziri viongozi wake wajiondoe wenyewe.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakurugenzi wa Makampuni 79, wakati akipokea gawio la Serikali kutoka kwa Makampuni hyo ambapo amepokea zidi ya Trilioni 1.

Rais Magufuli amesema; "Waziri tumebembelezana sana hatuwezi kukaa na viongozi ambao taasisi zao hazitoi gawio na pesa yetu ya Serikali inateketea kule.

“Hapa ni Mashirika 79 tu ndio yametoa gawio, hao wengine kila siku wanasema wanapata hasara lakini wana magari na vingine, Mashirika 187 hayana Habari ya kuchangia, lakini wana Bodi kuna Viongozi uko wanasafiri, wanastarehe na wanalipana posho


”Na yapo Mashirika ambayo mishahara yao inalipwa na Serikali, wamepewa hadi nyumba lakini hawajaleta gawio ungekuwa wewe Rais ungefanyaje?, ukute wengine wamelala Hotelini sasa hivi wanatuangalia kwenye TV

"Haiwezekani tukawa na watu walaji tu, hata mwanaume asipopeleka kitu nyumbani mwanamke anaweza kumfukuza, saa nyingine anaweza kumnyima ugali na hata saa nyingine anaweza kumnyima vyote mpaka mboga." ameongeza Rais Magufuli


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post