IRAN YATANGAZA HATUA MPYA ZA KUKIUKA MKATABA WA SILAHA ZA NYUKLIA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 5, 2019

IRAN YATANGAZA HATUA MPYA ZA KUKIUKA MKATABA WA SILAHA ZA NYUKLIA

  Malunde       Tuesday, November 5, 2019

Iran imetangaza leo hatua zake mpya za kukiuka makubaliano makubwa ya silaha za nyuklia yaliyosainiwa mwaka 2015 kati ya mataifa yenye nguvu kubwa duniani.


Iran imesema kwa sasa inatumia nyenzo ambayo ina kasi ya mara 50 zaidi ya ile iliyokubaliwa na mkataba huo. 

Tangazo hilo limetolewa wakati Iran ikianzisha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40, tangu Marekani ilipoukamata ubalozi wake mnamo mwaka 1979, mzozo uliodumu kwa siku 444. 

Mkuu wa shirika la kitaifa la nishati ya Atomiki nchini Iran Ali Akbar Salehi amesema kwa kuanza kutumia nyenzo hizo za kasi kubwa, Iran itapunguza muda wa mwaka mmoja ambao wataalam walisema Iran itauhitaji ili kuwa na vifaa vyote vya kutengeneza silaha za nyuklia endapo itaamua kufanya hivyo. 

Iran ilishakiuka makubaliano hayo kuhusu urutubishaji madini ya urani kama hatua ya kuushinikiza Umoja wa Ulaya kupata mkataba mpya, mwaka mmoja tangu Marekani ilipojiondoa katika mkataba huo.

-DW


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post