RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA 'WASAA WA MARAFIKI WA HABARI MKOA WA MWANZA' | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, November 9, 2019

RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA 'WASAA WA MARAFIKI WA HABARI MKOA WA MWANZA'

  Malunde       Saturday, November 9, 2019
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amefungua mkutano wa wasaa wa marafiki wa Habari mkoani Mwanza ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Habari Mkoa Mwanza (MPC).

Akifungua mkutano huo Novemba 09, 2019 jijini Mwanza, Mongella amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari hivyo itaendelea kushirikiana na wabahabari katika kuchochea maendeleo.

Aidha Mongella ameipongeza MPC kupitia Mwenyekiti wake Edwin Soko kwa kuandaa mkutano akisema utasaidia kujadili fursa mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo ukarabati na ujenzi meli mpya katika Ziwa Victoria pamoja na ujio wa reli ya kisasa (SGR) huku ukitoa picha halisi katika kuelekea kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Biashara mkoani Mwanza utakaofanyika mwaka ujao.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano baina ya vyombo vya habari na wadau katika kufanikisha ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza huku akisisitiza wanahabari kufanya kazi kwa weledi ili kulinda mustakabali wa amani kwa Taifa.

Mkuu wa Mkoa Mwanza,John Mongella akizungumza wakati akifungua mkutano huo

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kushoto ni Florah Magabe ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Nyamagana.

Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akizungumza wakati wa mkutano huo.

Wanahabari na marafiki wa habari wakifuatilia mkutano huo.

Mkutano unaendelea

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post