MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIGO CHEMSHA BONGO APATIKANA


Mtaalam wa Huduma za ziada-Tigo, Fabian Felician na Jehud Ngolo- Afisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. wakimpigia simu Shaban Khamis Ali,mkaazi wa Zanzibar, mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha bongo
Mtaalam wa Huduma za ziada-Tigo, Fabian Felician na Jehud Ngolo- Afisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. wakimpigia simu Shaban Khamis Ali,mkazi wa Zanzibar, mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha bongo

****
Droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Tigo Chemsha Bongo’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkaazi wa Zanzibar, Shabani Khamis Ali (48) amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID yenye thamani ya 23m/-. Khamis akiongea baada ya kupigiwa simu na Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindi kupitia promosheni hiyo kwa kujishindia gari mpya. 

“Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunifungia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari, kwani itanisaidia katika mizunguko yangu ya kibiashara “alisema kwa furaha. 

Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo. 

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumpata mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid,yenye thamani ya 23m/-, gari hili ni jipya kabisa, baada ya kumpata mshindi taratibu zengine zitafata ili tuweze kumkabidhi Shaban Khamis Ali gari lake jipya. Tunawashukuru wateja wetu kutoka nchini pote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”. alisema Felician. 

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako  imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali. 

Kwa kumalizia Felician aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527