APPS 20 HATARI UNAZOSHAURIWA KUZIONDOA KWENYE SIMU YAKO HARAKA

Watumiaji wa Android wamepewa orodha ya apps za kuziondoa kwenye simu zao kwa sababu za kiusalama wa data na kuondoa matangazo yanayotokea sehemu zisizohusika kwenye simu zao.

Ushauri huo umetolewa na watafiti kutoka ESET ambao wamegundua app 42 kwenye soko la Google Play Store ambazo zimekuwa zinakuja na mfumo wa kimatangazo usio rasmi – adware. Mfumo huo una sababisha betri ya simu kuisha haraka, utumiaji wa data – intaneti na ata kuchukua taarifa zako binafsi kwenye simu.

Baada ya utafiti wa ESET kuweka wazi Google waliondoa apps hizo kwenye soko lao la Apps, ila inakuitaji wewe kuziondoa mwenyewe. Pia kuzifahamu ni muhimu kwa watu ambao wanatumia masoko mengine ya apps nje ya soko la Google Play Store. Apps hizo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 8.

Apps hizo zinauwezo wa kuonesha matangazo ata kama simu imefungwa (locked) kitu ambacho huwa kinapigwa na Google, kwani kufanya hivyo kuna sababisha utumiaji mkubwa wa betri na nje ya makubaliano yao na watengenezaji wa apps.

Apps hizo ni: Smart Gallery, SaveInsta, Mini lite for Facebook, Free Radio FM Online, Free Video Downloader, Free social video downloader, File Downloader, Water Drink Reminder, Smart Notes for You, DU Recorder, Tank classic, Heroes Jump, Solucionario, Ringtone Maker, Video downloader, Ringtone Maker Pro, Basketball Perfect Shot, HikeTop+, MP4 video downloader, Flat Music Player, Free Top Video Downloader.

Pitia orodha vizuri  hapo chini na kama kuna app bado unaitumia unashauriwa kuiondoa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527