SHULE YA SEKONDARI ORKEESWA YA JIJINI ARUSHA YANG'ARA MICHEZO YA SHULE ZA KIMATAIFA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 26, 2019

SHULE YA SEKONDARI ORKEESWA YA JIJINI ARUSHA YANG'ARA MICHEZO YA SHULE ZA KIMATAIFA

  Malunde       Tuesday, November 26, 2019

Ndajiri Lonyori kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mchezo wa mpira wa kikapu wa wasichana chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 
Ndajiri Lonyori kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa netball chini ya miaka 15 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Amani Isaya kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa volleyball chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 
Emmanuel Meibuko golikipa wa timu ya shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mpira wa miguu wa wavulana chini ya miaka 19 baada ya kuibuka washindi kwa goli 3 - 2 katika mechi iliyokuwa ngumu sana kwa vijana hao wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 

Shule ya Sekondari Orkeeswa iliyopo mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali ya Shule za Kimataifa. 

Shule hizo kutoka mikoa mbalimbali nchini zilikutana mkoani Kilimanjaro na kuchuana vikali katika michezo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa miguu, tennis, swimmings, netball, volleyball, frisbie, rugby na michezo mingineyo. 

Timu za kikapu U19 wasichana na U19 wavulana pamoja na timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo zilionekana kuwa imara zaidi baada ya kushinda kwa kishindo timu za shule mbalimbali zilizo pambana nao. 

Shule za kimataifa nchini zilikuwa na wikiendi ya michezo iliyoanza mwishoni mwa wiki,Ijumaa na kufikia tamati Jumapili. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post