TUNDU LISSU ASITISHA SAFARI YAKE YA KURUDI NCHINI


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, amesema amesimamisha kwa sasa mpango wake wa kurejea nchini Tanzania mpaka hapo usalama wake utakapohakikishwa na Viongozi wake wa CHADEMA.


Tundu Lissu ametoa kauli hiyo jana Jumatano Oktoba 9 katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Sauti ya Marekani (VOA) baada ya kuulizwa swali na mtangazaji Mwamoyo Hamza kuhusu mpango wake wa kurejea nchini baada ya kumaliza matibabu.

“Nimeshakamilisha tiba kwa hiyo sababu ya kiafya ya kuendelea kukaa Ubelgiji haipo tena, iliyobaki sasa ni viongozi wenzangu (wa Chadema) waliopo Tanzania waniambie mazingira yapo sawasawa ya kiusalama ya mimi kurudi.

“Kumbuka wale walionipiga risasi 16 mchana wa saa saba bado wanaitwa watu wasiojulikana.

“Nimebadili kauli kwa sababu za wazi nilizozisema. Mazingira ya kiusalama si mazuri kwangu. Kuna maneno yanajitokeza kwenye mitandao ya kijamii kwamba ngoja aje  . Sasa katika mazingira haya watu wenye busara wakasema hebu tuangalie hali ya usalama” ,alisema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527