TANZANIA KUNUFAIKANA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIANINFRASTRUCTURE INVESTMENT’

Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. 


Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527