SHIRIKA LA NDEGE LA TANZANIA (ATCL) LASITISHA SAFARI ZA KWENDA AFRIKA KUSINI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, October 6, 2019

SHIRIKA LA NDEGE LA TANZANIA (ATCL) LASITISHA SAFARI ZA KWENDA AFRIKA KUSINI

  Malunde       Sunday, October 6, 2019

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limesitisha rasmi safari zake kati ya Dar es Salaam na Johanesburg, Afrika Kusini kuanzia Oktoba 7, 2019 na abiria mbao tayari walikuwa wamekata tiketi kuanzia siku hizo watarudishiwa nauli zao.

Taarifa iliyotolewa na ATCL Oktoba 3, 2019 na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi iliwaelekeza mawakala wa tiketi wote kurejesha nauli za wateja hao ambao tayari walikuwa wamekata tiketi.

ATCL ambayo ilikuwa ikifanya safari hiyo mara nne kwa wiki (Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili) iliacha kufanya safari kati ya miji hiyo Agosti 23,2019 baada ya ndege yake aina ya Airbus A220-300 kuzuiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jiji Johanessburg kwa amri ya mahakama kuu ya Guateng.

Baada ya takribani wiki mbili ndege hiyo iliachiwa huru kwa uamuzi wa mahakama.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post