AUAWA KWA KUPIGWA RISASI YA MAKALIO KAHAMA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kijana aliyekutwa na Kitambulisho chenye jina la Mishael Masatu (29) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kwenye makalio na mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi Serengeti Security Services Ltd, mkazi wa mtaa wa Malunga kwenye yard ya magari katika kisima cha mafuta cha PetroAfrica mtaa wa Mbulu Mjini Kahama.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Oktoba 16,2019 majira ya tisa alfajiri.

"Mlinzi wa kampuni ya Ulinzi ya Serengeti Security Services LTD  Isumail Hassan (20) mkazi wa mtaa wa Malunga akiwa kazini hapo kisimani, alifyatua risasi moja kutoka kwenye bunduki aina ya Shortgun yenye namba HP.9-1.  007710112 mali ya Kampuni ya Serengeti Security Services LTD na kumjeruhi matakoni mtu aliyekutwa na kitambulisho chenye jina la Mishael Z. Masatu(29), mkazi wa Nyihogo mtaa wa Sazia ambaye aliingia kwenye yard hiyo bila kibali",ameeleza Kamanda Abwao.

 "Chanzo cha tukio ni majeruhi kuingia kwenye yard bila kibali na kudhaniwa kuwa ni mwizi. majeruhi alianza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama na baadaye alifariki dunia",amesema Kamanda Abwao.

Amesema askari mlinzi  anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya Kahama wakati upelelezi unaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527