ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020


HESLB imetoa orodha ya waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zina upungufu ili wafanye marekebisho kwa siku nne kuanzia  Jumatatu tarehe 30 Septemba 2019 ambapo pia mwongozo wa jinsi ya kufanya marekebisho utatolewa.

Hatua ya HESLB inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo imebainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.

Orodha hii ni ya wanafunzi wanaokwenda kusoma masomo ya Shahada ya kwanza. Orodha ya waombaji mikopo watakaojiunga na Shule ya Sheria (Law School of Tanzania), Shahada za Uzamili na Uzamivu itatolewa kesho Jumatatu tarehe 30 Septemba 2019.

Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika *bofya hapa.*

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527