KABENDERA AMUOMBA RADHI RAIS MAGUFULI

Mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera amemwomba radhi Rais na Serikali ya nchi hiyo akiomba kusamehewa kama kuna makosa ameyafanya.


Kabendera amesema hayo leo Jumanne Oktoba 1, 2019 jijini Dar es Salaam kupitia kwa wakili wake, Jebra Kambole.

Kambole amesema hayo muda mfupi baada ya kesi inayomkabili mwandishi huyo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha Sh173.24 milioni kuahirishwa hadi Oktoba 11, 2019 kutokana na upelelezi kutokamilika.

“Sisi kama mawakili tunatoa ombi kwa Rais, kama Erick katika utendaji kazi wake kama kuna mahali alimkosea Rais au Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba yake, familia yake, ndugu zake tumwombe radhi,” amesema Kambole

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam, alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527