Breaking : BASI LA ALLY'S STAR LAUA AFISA WA MANISPAA YA SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 1, 2019

Breaking : BASI LA ALLY'S STAR LAUA AFISA WA MANISPAA YA SHINYANGA

  Malunde       Tuesday, October 1, 2019
Mhoja Mambosasa enzi za uhai wake.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Fundi Sanifu wa Majengo 'mchoraji ramani za majengo' wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhoja Mambosasa (56) amefariki dunia baada ya kugongwa na Basi la Kampuni ya Ally's Star  eneo la Kituo cha Mabasi ya Kampuni hiyo iliyopo karibu na Stesheni barabara kuu ya Mwanza- Shinyanga.
Ajali hiyo imetokeo leo Jumanne Oktoba 1,2019 majira yaa saba na dakika 50 mchana katika eneo la Ofisi ya Mabasi ya Kampuni ya Ally's iliyopo Mjini Shinyanga barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza.

Akizungumza na Malunde1 blog,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

"Taarifa nilizopewa ni kwamba Mfanyakazi wetu Mhoja Mambosasa ambaye ni fundi sanifu majengo 
alikuwa kwenye shughuli zake kwenye ofisi za Mabasi ya Allys, wakati anatoka kuelekea ofisini akiendesha pikipiki ndipo akagongwa na basi la Allys lililokuwa linaingia kituoni",amesema Mwangulumbi.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Audax Majaliwa  amesema gari hilo lenye namba za usajili T622 AME aina ya Scania Bus mali ya Yahaya Amor likiendeshwa na Musa Said (40) mkazi wa Mwanza lilimgonga mwendesha pikipiki yenye namba za usajili T843 BBM SANLG aitwaye Mhoja Mambosasa ambaye ni Afisa Mpango miji wa Manispaa ya Shinyanga.

"Mhoja Mambosasa amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga",amesema Kamanda Majaliwa.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kukata kona kutaka kuingia njia ndogo kutokea njia kuu bila kufuata sheria za usalama barabarani.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post