NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE.KANYASU AWATAKA WAZAZI WATIMIZE WAJIBU WAO


Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewakumbusha Wazazi wenye watoto waliowapeleka kusoma katika shule binafsi wahakikishe wanawatimizia mahitaji yao ya muhimu katika kipindi chao chote cha masomo ili waweze kufaulu mitihani yao ya mwisho.

 Badala ya kuja na  zawadi nyingi siku ya mahafali ajili ya kuwapongeza wanapohitimu  ilhali wanafunzi hao walikuwa wakirudishwa nyumbani kila wakati wakachukue ada ya shule.

Ametoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa wanafunzi  60 yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Rocks Hill iliyopo katika wilaya ya Ilemela  jijini Mwanza.

Amesema wazazi lazima wawekeze kwa watoto wao ili waweze kusoma katika mazingira ya kutokuwa na hofu ya kurudishwa nyumbani kwa sababu wazazi wao  hawajawalipia ada ya shule.

"Ukiamua kumsomesha mtoto lazima ukubali kwamba elimu haijawahi kuwa bure, hivyo ni jukumu la kila   mzazi kukidhi mahitaji ya mwanae likiwemo suala la  kumlipia ada kwa wakati." alisisitiza Kanyasu

Amesema ni vyema wazazi hao kutambua dhamana waliyonayo katika kuwandaa watoto wao kielimu badala ya kusubili hadi watoto  warudishwe nyumbani.

Mhe.Kanyasu amesema kitendo hicho cha wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa ajili ya ada kimekuwa kikiwarudisha nyuma kimasomo kwa vile wamekuwa wakikosa baadhi ya vipindi.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiweze kuharibikiwaa mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Meshak Mpalanga amesema katika kipindi chao chote cha masomo wamelelewa kimaadili hali itakayowasaidia kupambana zaidi katika kuyamudu maisha

Akizungumzia jinsi walivyoandaliwa kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho, Amesema anatarajia idadi kubwa ya wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano.

NayevMwanafunzi bora katika masomo yote aliyetajwa katika mahafali hayo, Diana Titus amesema wamejianda vyema na wapo tayari kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho.

" Tunawashuru walimu wote kwa kutulea na kutufundisha, tunaamini sote tutafanya vizuri mitihani yetu.alisisitiza Mwanafunzi huyo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527