Picha : BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA...MKURUGENZI AGAWA CHAKULA KWA WATEJA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, October 7, 2019

Picha : BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA...MKURUGENZI AGAWA CHAKULA KWA WATEJA

  Malunde       Monday, October 7, 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiwahudumia baadhi ya wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amewaongoza baadhi ya watendaji wa benki hiyo kugawa chai kwa wateja wao.

Akizungumza akiwa kwenye tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Nsekela alisema ni wiki muhimu kwa wateja wa CRDB.

Alisema ni wiki ya viongozi wa benki hiyo kutoka matawi yote kuwafuata na kuwahudumia wateja kwa upendo chini ya kaulimbiu ya 'Ulipo tupo kukupa Magic'.

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani kauli mbiu ya dunia ni 'The magic of service' na sisi benki yetu tunashiriki kwa kuwahudumia wateja wetu.

"Tunawaambia ulipo tupo kukupa Magic. Tumeandaa vitu vingi vizuri naamini wateja wetu watafurahia," alisema Nsekela.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, TullyEsther Mwambapa, alisema wafanyakazi wa benki hiyo watafanya shughuli za kijamii kwa kushtukiza na kuwashukuru wateja wao.

"Ni wiki hii ya huduma kwa wateja, tunaitumia kushukuru wafanyakazi wetu kwa huduma wanazozitoa na kushukuru wateja wetu kwa kutuchagua.

"...Tutawafikia na kuwahudumia wateja wetu kwa kuwashtukiza hivyo wajiandae kwa mambo mazuri," alisema Mwambapa.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post