MAKONDA AWAKABIDHI SUMA JKT UJENZI HOSPITALI UBUNGO

Kitengo cha uzalishaji mali cha Jeshi la kujenga Taifa (suma JKT), kimepewa kazi ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ubungo.

Kazi hiyo wamepewa na jana Oktoba 29, 2019 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye amesema kuwa ujenzi huo unatakiwa kamilika kwa miezi mitatu.

Amebainisha hayo jana alipotembelea eneo itakapojengwa hospitali hiyo Kimara Baruti, ambapo aliambatana na viongozi wengine na kuangalia jinsi maandalizi mbalimbali yalivyoanza kufanyika.

Makonda ametoa shukrani zake kwa mara nyingine tena kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kukubali ombi lake la sh 1.5 bilioni za ujenzi wa hospitali hiyo.

” Wilaya hii ni mpya inahitaji viongozi shupavu wa kuwaletea maendeleo, ni kazi ya viongozi wanaochaguliwa na wananchi.

“Kwa bahati mbaya Ubungo ilipata viongozi wanaojali matumbo yao tu. Hata leo hapa hawapo ila kesho watakuja na maneno matamu ili muwape kura” Alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Mkurugenzi mtendaji wa Suma JKT, Kanali Rajabu Mabele amesema kuwa watahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527