RAS TANGA NA DC KOROGWE WATEMBELEA ENEO LA MANDERA KUONA MAFURIKO YALIYOSABABISHA BARABARA KUFUNGWA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, October 14, 2019

RAS TANGA NA DC KOROGWE WATEMBELEA ENEO LA MANDERA KUONA MAFURIKO YALIYOSABABISHA BARABARA KUFUNGWA

  TANGA RAHA BLOG       Monday, October 14, 2019
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa wametembelea eneo la Mandera linalounganisha wilaya za Korogwe na Handeni na kujionea mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda
Katibu Tawala  wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi (aliyesimama mbele kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi alipotembelea kuona athari za mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda, kulia mbele  ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa. Octoba 13,2019
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa.(Kulia mbele) akiwapa pole wakazi wa wilaya ya Korogwe pamoja na wananchi wote walioshindwa kuendelea na Safari kutokana na maji kujaa katika eneo hilo la Mandera kushoto mbele ni Katibu Tawala  wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
 Hili ndilo eneo la Mandera ambapo daraja lilifungwa kwa muda 
Maji yakiwa yamezidi daraja , ingawa hapa maji yanaonekana kupungua kiasi
Hali ya mafuriko ilivyokuwa katika eneo la Mandera
Mhe. Kissa G. Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe (wa tatu kutoka kushoto) akimonesha jambo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi walipotembelea eneo la mafuriko.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akisisitiza  jambo walipotembelea eneo la mafuriko.

Picha na Fredy Njeje - Korogwe

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post