WAZAZI MKOANI MWANZA WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka
mitano kwenye Vituo vya Afya kupata chanjo bure hidi ya magonjwa ya Surua, Rubella na Polio kuanzia tarehe 17-21 Oktoba 2019.

Kwa Mkoa Mwanza, zaidi ya watoto laki sita (watoto 637,579) wanatarajiwa kupewa chanjo ya Rubella na Polio huku
watakaopewa chanjo ya Surua wakitarajiwa kuwa zaidi ya elfu sitini (watoto 266,140) hivyo kufanya jumla ya watoto wanaotarajiwa kuchanjwa kuwa laki tisa elfu tatu mia saba kumi na tisa (watoto
903,719). 

Kitaifa uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika mkoani Morogoro, Oktoba 17,2019.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Surua, Rubella na Polio.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akitoa salamu za Wizara kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo mkoani Mwanza.
Tazama Video hapa Chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527