CHADEMA WATOA KAULI KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawatasusia uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Novemba 24 mwaka huu na amewataka viongozi, wanachama na Watanzania kuhamasishana kujiandikisha.

Amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi ambapo ameeleza  uchaguzi huo ndio unawaleta viongozi wanaokwenda kutatua changamoto za wananchi hivyo kuacha serikali ifanye uamuzi ni kosa.

“Tunapaswa kuweka kando tofauti zetu, twendeni kwa wingi tukajiandikishe ili tushiriki kwenye uchaguzi huu muhimu,” amesema Mbowe

Ameendelea kwa kusema wananchi kusuasua kwenda kujiandikisha ni matokeo ya kile alichodai kuwa ni serikali  kuweka msisitizo katika kuwazuia watu wa upinzani kufanya mikutano ya kisiasa.


“Ni makosa makubwa na aibu kususia. Kwa muda wa siku tatu zilizoongezwa, viongozi wote wa kada zote, wahamasishane watoke kwa wingi kwenda kujiandikisha, hatuna sababu za kususia kwani tutakuwa tumesusia maisha yetu,” amesisitiza Mbowe

“Tunakwenda kushiriki uchaguzi huu na tutashinda, hatutakuwa woga na haya ni mapambano ya kisiasa, tutatumia nguvu za umma kuhakikisha tunashinda uchaguzi huu.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527