VIKAO VYA BUNGE LA TANZANIA KUANZA OKTOBA 21

Vikao vya Kamati 14 za Kudumu za Bunge, vinatarajia kuanza tarehe 21 Oktoba 2019 hadi Novemba Mosi mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 16 Oktoba 2019 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Ofisi ya Bunge.

Taarifa hiyo imeleeza kuwa, miongoni mwa shughuli zitakazofanyika katika vikao hivyo, ni uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Pia, Kamati hizo zitafanya uchambuzi wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma katika mashirika na taasisi mbalimbali nchini.

Na uchambuzi wa Sheria ndogo zilizowasilishwa wakati wa mkutano mkuu wa kumi na sita wa Bunge.Pamoja na Kupokea na kujadili taarifa ya mapendekezo ya mwongozo wa kutayarisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527