WATU 41 WAKAMATWA NA POLISI NCHINI AFRIKA KUSINI KWA KUVAMIA, KUPORA NA KUCHOMA MOTO MADUKA YA WAHAMIAJI TOKA MATAIFA YA AFRIKA

Watu 41 wamekamatwa na Polisi nchini Afrika kusini kwa madai ya kupora mali na kuchoma maduka ya Wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika.Mamia ya wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakionekana wakikimbia na kupora mali za watu tangu Jumapili  katika eneo lenye shughuli za kibiashara na kuchoma moto maduka yanayoaminiwa kumilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika.

Ghasia hizo zilianzia katika eneo la Jeppestown, lililopo katika wilaya ya kati yenye shughuli za biashara. Lakini zilisambaa hadi kwenye maeneo mengine kama vile Denver, Malvern, Turffontein, Tembisa na maeneo mengine ya vitongoji vya jiji la Johansburg.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post