RUBANI AZIRAI NDANI YA NDEGE WAKIWA ANGANI.... MWANAFUZI ASHIKA USUKANI NA KUTUA SALAMA


Rubani mwanafunzi nchini Australia ametua ndege salama baada mwalimu wake kuzirai akiwa angani.

Max Sylvester, makazi wa Australia magharibi aliwasiliana kwa dharura na waelekezaji wa ndege saa moja baada ya mwalimu wake kuzirai wakiwa angani juzi Jumamosi iliyopita Agosti 31.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, wahudumu hao walimsaidia mwanafunzi huyo kutua ndege salama katika Uwanja wa Ndege wa Perth.

Sylvester alisifiwa kwa kuchukua hatua ya haraka na kuwa mtulivu wakati wa tukio hilo.

Katika mawasiliano yaliorekodiwa na baadae kuwekwa wazi kwa umma, Slivester alielezea hali ya mwalimu wake kabla ya kuchukua jukumu la kupaisha ndege hiyo.

“Kwanza aliniegemea katika bega langu, nilijaribu kumuamsha lakini aliangua,” mwanafunzi huyo aliwaambia mafundi wa mitambo.

Alipoulizwa kama anajua jinsi ya kupaisha ndege aina ya Cessna mwanafunzi huyo alijibu “hili ni somo langu la kwanza.”

Baada ya kupaa juu ya Uwanja wa Ndege wa Perth kwa karibu saa moja akifuata maagizo ya jinsi ya kutua, hatimae alitua salama huku maafisa wa kukabiliana na hali ya dharura pamoja na familia yake wakimsubiri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527