TETESI ZA SOKA LEO JUMANNE SEPTEMBA 3,2019

Ujumbe mfupi kutoka kwa Lionel Messi huenda ulivuruga mpango wa Barcelona kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, kutoka klabu ya Paris St-Germain. (L'Equipe, via Star)

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi angelifanikiwa kumpata Neymar msimu huu ikiwa dau la kuvunja rekodi la euro milioni 300 sawa (£272m) lingemfikia. (Le Parisien, via Sport)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, yuko radhi kuhamia Manchester United baada kukiri kuwa "angelipendelea" kurejea England. (Mirror)Jadon Sancho, Mshambuliaji wa Borussia Dortmund

Mshambuliaji wa Croatia Ante Rebic, 25, amejiunga na AC Milan kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili kutoka Eintracht Frankfurt, huku mshambulizi Andre Silva, 23, akitarajiwa kuchukua nafasi yake . (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji Atletico Madrid Mcroatia Nikola Kalinic, 31, amaejiunga na Roma kwa mkopo wa msimu mzima huku klabu hiyo ya Serie A ikimtuma mshambuliaji wa Czech Patrik Schick, 23, kwa mkopo kwenda RB Leipzig. (Gazzetta dello Sport - in Italian)Mshambuliaji Atletico Madrid Mcroatia Nikola Kalinic

Kiungo wa safu ya kati wa Mbrazil Rafinha Alcantara, 26, amesaini kandarasi ya kurefusha mkataba wake na Barcelona kabla ya kujiunga na Celta Vigo kwa mkopo utakaodumu msimu mzima. (Marca)

Mchezaji wa kiungo cha kati Mbelgiji Steven Defour, 31, ametia saini mkataba wa kujiunga na Royal Antwerp siku mbili baada ya kuafikiana na Burnley kuvunja mkataba wake. (Het Laatste Nieuws - in Dutch)

Winga wa Leicester Mualgeria Rachid Ghezzal, 27, amesema "nafurahi sana" kuwa katika nafasi ya kuhamia Fiorentina kwa mkopo. (Leicester Mercury)

Atalanta imemsaini beki Mholanzi Simon Kjaer, 30, kutoka Sevilla kuchukua nafasi ya mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel, ambaye mkataba wake ulivunjwa siku 24 baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Serie A. (Goal)Winga wa Leicester Rachid Ghezzal

Winga Marcus Edwards,20, ambaye wakati mmoja alibatizwa jina la'Messi mdogo' amehama Tottenham. (Sun)

Vilabu vya Ligi kuu ya Premia huenda vikaungana kushinikiza dirisha la uhamisho wa wachezaji msimu ujao uendane na ule wa Ulaya. (Telegraph)

Beki wa kusho wa Leeds Mbelgiji Laurens de Bock, 26, amesema kutazama filamu ya 'Sunderland 'Til I Die' kulimsaidi katika kufanya uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo ya League One. (Sun)
Tetesi Borsa JumatatuNeymar

Barcelona imesitisha jaribio lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar kutoka Paris Saint-Germain hadi msimu ujao. (ESPN)

Mazungumzo kati ya vilabu hivyo yalivunjika baada ya PSG kulegeza masharti yao licha ya Neymar kujitolea kulipa £17.7m kufikia makubaliano ya usajili wake

Roma wanamatumaini ya kummsaini kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ,30. (Sky Italy - in Italian)Henrikh Mkhitaryan, Kiungo wa kati wa Arsenal

Juventus bado wana matumaini ya kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona wa miaka 31 Mcroatia Ivan Rakitic - na huenda wakatoa ofa ya kumuachilia mchezaji wa kiungo cha kati Mjerumani Emre Can, 25, kama sehemu ya kufikia mkataba wa kumsajili Ivan Rakitic. (Sport - in Spanish)

Mlinzi wa Bayern Munich Mjerumani Jerome Boateng, 30, anakaribia kujiunga na mabingwa wa Italia, Juventus. (Bild, in German)
PSG wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 26, kwa mkopo kutoka Inter Milan. (RMC Sport - in French).
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527