MAJIOLOJIA WATUA SHINYANGA KUCHUNGUZA KILE KINATAJWA KUWA VOLCANO NDEMBEZI





Umesikia kuhusu uwepo wa dalili za Volcano katika eneo la Ndembezi Mazinge Manispaa ya Shinyanga hali iliyozua hofu kwa wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo??

Kutokana na hali hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki mbili sasa,tayari Wataalamu wa Jiolojia wametua Shinyanga ili kufanya uchunguzi....

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Diwani wa Kata ya Ndembezi,David Nkulila amepost ujumbe ufuatao




#MAJIOLOJIA WAMEFIKA LEO ENEO LENYE TOPE
INAYOVUJA KATA YA NDEMBEZI - MTAA WA NDEMBEZI NA MTAA WA TAMBUKARELI (Mazinge) .
Namshukru Mh D.C. Wilaya ya Shinyanga mjini Yasinta Mboneko kwa ukaribu wa kipekee kwetu sote #WanaNdembezi katika kuhakiksha tunakua SALAMA kwa kuzuia watu kufika eneo hilo ambalo linalotishia USALAMA kutokana na Dongo lililopanda toka chini na lenye ubichi tekeke katikati ya njia ya mto, sambamba na rojo ya tope inayobubujika toka chini ambayo hiyo ipo ng'ambo(Mtaa wa Ndembezi )
Leo amekuja na #majiolojia ambao, ni wataalamu zaidi wa mambo hayo na kukagua eneo pamoja na kuchukua sampo (#Specimen )kwa ajili ya kwenda kufanyia uchunguzi wa kina na kuahidi kuleta taarifa ya uchunguzi mapema kwa D.C. na kwingine(Wazi-- itakua kwa Mh RC)
Pamoja na kutuondolea hofu wataalamu hao juu ya tukio hilo, bado wameunga mkono tamko la D.C. Kuzuia WANANCHI kuzagaa jirani na maeneo hayo kwamba si salama,Kumbe tahadhari ni jambo muhimu.
#ONYO limetolewa kutosogea eneo hilo na Mh D.C. Yasinta Mboneko, ni vema tukazingatia kwa usalama wa maisha yetu .#KUPUUZA ni kutenda kosa la makusudi na kuweka rehani maisha yako. Endapo serikali itabaini upo usalama wa kutosha au vinginevyo, mtajulishwa.Tukumbuke #SUMUHAIONJWI. Kinga daima inatija kuliko tiba. Tuache pia uzushi unaovuruga AMANI na utulivu. Busara kutoeleza usichokijua.Serikali inajali maisha yetu ambayo ni Pamoja na usalama wetu.
#Zingatia.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527