HOFU YA MLIPUKO WA KILE KINATAJWA VOLCANO YAENDELEA KUTANDA NDEMBEZI SHINYANGA....UJI UJI UNAVUJA KUTOKA ARDHINI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 19, 2019

HOFU YA MLIPUKO WA KILE KINATAJWA VOLCANO YAENDELEA KUTANDA NDEMBEZI SHINYANGA....UJI UJI UNAVUJA KUTOKA ARDHINI

  Malunde       Thursday, September 19, 2019

Watalaamu wa Jiolojia na Miamba wameombwa kufika katika eneo la Mtaa wa Mazinge kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kuangalia hali kufuatia uwepo wa kile kinachodaiwa kuwa ni mlipuko wa Volcano iliyolala ambayo imezua taharuki kwa wakazi wa kata hiyo baada ya kutoa uji uji tope hali iliyoleta wasiwasi kwa wakazi wa jirani.Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Mazinge ambapo limetokea tukio hilo wamesema kuwa hali hyo imetokea baada ya kuona tope zito likitoka kutoka chini ya ardhi na kuja juu mfano wa uji hali ambayo imewapa shaka huku wengine wakisem kuwa kumewakupo tamaduni za siku nyingi ambapo hali hyo hutokea baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya matambiko


Nao baadhi ya viongozi waliofika katika eneo hilo wakiwemo wakurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi na Michael Matomola wa Ushetu wamesema zinahitajika jitahada za haraka za watalaam wa jiolojia kufika haraka eneo ilo ili kubainisha kama hali inaweza kuwa na athari kwa jamii za maeneo hayo ili waweze kupewa tahadhari kulingana na hali hiyo.
Uji uji huo upo ng'ambo ya mto unaotenganisha Ndembezi na Tambukareli na ambapu kuna udongo unaoonekana kama uji uliobubujika kutoka chini,umeziba njia ya mto.

Kwa Mujibu wa Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila aliyefika mapema Septemba 16,2019 eneo la tukio alisema uji uji huo  ni dalili ya Volcano lakini jinsi ilivyo kuna baadhi ya watu wanaingiza mambo ya mila kwamba ni Mizimu la Malembela

Amesema Taharuki iliyopo ni wananchi kuhofia kuwa huenda Volcano ikalipuka na kuleta athari lakini wamewapa elimu wananchi kuendelea kuwa na subira serikali inalifanyia kazi watalaamu watatoa  majibu .

"Kuna uji unatoka,kuna kama kashimo kanatoa uji laini kama kanasukumwa hivi...Tunasubiri majibu kutoka serikalini,tuendelee kuwa na subira kulikoni kuendelea kuzungumzia kitu ambacho hatuna uhakika nacho
VOLCANO AU NINI?
MTONI- MPAKA KATI YA TAMBUKARELI NA MTAA WA NDEMBEZI KATA YA NDEMBEZI!
Baada ya kupewa taarifa na Mwenyekit wa Mtaa wa Ndembezi juu ya kilichotokea hapo.Nimefika asubui leo na kujiona Ujiuji laini uliobubujika toka chini ardhini na lundo la udongo uliojilundika katikati ya mto huo na kuziba njia ya mto (Pichani)
#UFUMBUZI. Nimeongea na Mh D.C. Yasinta Mboneko na anatuma wataalamu hapo na ndio watakao toa majibu sahihi ya kitaalamu na hata ushauri.Tafadhari tuache taharuki na kuelezea tusicho kijua. Tuwe na subira na tahadhari hasa kwa watoto.Serikali inalishughulikia.
Udongo uliokauka mtoni
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi (katikati) akiangalia uji uji huo
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post