MCHUNGAJI LUGAKINGIRA : VIONGOZI TUMIENI ULIMI VIZURI KUEPUKA MIGOGORO


Mchungaji Gabriel Lugakingira 

Na Lydia Lugakila -Malunde 1 blog 
Waumini wa madhehebu mbalimbali,viongozi wa dini na viongozi wa serikali mkoani Kagera wametakiwa kujihadhari na matumizi ndimi zao ili kuepuka na kauli zinazoweza kusababisha migogoro isiyoisha katika jamii na nchi kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa leo Septemba 8, 2019 na Mchungaji Gabriel Lugakingira wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania KKKT mtaa wa Ibura  wakati wa ibada ya Jumapili ilikwenda sanjari na maombi maalumu kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani kuhitimu darasa la saba mwaka 2019.

Mchungaji Lugakingira amesema muumini yeyote ama kiongozi yeyote anayetumia vibaya ulimi wake kwa kutoa kauli mbovu na kashfa ni chanzo kikubwa cha kuwepo kwa migogoro isiyoisha.

"Naomba tuchunge sana mdomo unaotoa kauli,mdomo unaweza kuunganisha watu na unaweza kufarakanisha ,tujihadhari na matumizi mabaya ya ndimi zetu",amesema.

Ameeleza kuwa ulimi huo huo umesababisha hata kudharauliana kiimani na hata kuchochea ubinafsi na jitihada za wanadamu zimeshindwa kuleta mafanikio katika dunia kutokana na kutumia ndimi vibaya huku akihimiza kutoka katika mitihani ya Ibilisi na kufuata mitihani ya Mwenyezi Mungu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527