TIGO YAZINDUA PROMOSHENI YA TIGO CHEMSHA BONGO,KANDA YA ZIWA


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, wakati wa ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta Saizi Yako na bahati nasibu ya Tigo chemsha bongo, kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya na Afisa Huduma za Ziada wa Tigo Fabian Felician. 
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu gari atakalopewa mshindi wa Tigo chemsha bongo jijini Mwanza, wakati wa ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta Saizi Yako na bahati nasibu ya Tigo chemsha bongo. 
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati,akiwasha gari la mfano atakalopewa mshindi wa Tigo chemsha bongo jijini Mwanza, wakati wa ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta Saizi Yako na bahati nasibu ya Tigo chemsha bongo. 
****
 Mteja wa Tigo  kuzawadiwa gari aina ya Renault Kwid na wengine kujishindia mamilioni kama zawadi katika promosheni iliyozinduliwa leo Mwanza,iitwayo Tigo Chemsha Bongo katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako.


Akizungumza na waandishi wa habari,(Septemba 24,2019), wakati wa uzinduzi wa shindano la Tigo Fiesta  Chemsha Bongo, ambalo linatafanyia Tanzania nzima katika msimu wa Tigo, Mkurugenzi Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati, alisema kwa mara ya kwanza, mkoa huo umeweka historia ya kufungua shughuli zote za Tigo Fiesta Saizi Yako 2019

“Tunatambua umuhimu wa tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, kwamba si tu linaleta burudani kwa taifa bali linaibua na kukuza vipaji vipya hususan kwa tasnia ya muziki nchini,” alisema Madati.

Alisema tamasha hilo pia linasaidia katika kutoa elimu ya ujasiriamali lakini pia kutoa fursa mbali mbali kwa vijana.
Aidha Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya mkoa kwa ushirikiano wake wakati wote wa tamasha hilo na mengine mengi na kwamba hilo limesaidia kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi lakini pia kwa kujiamini. Katika hatua nyingine, Madata aliarifu kwamba kwenye shindano hilo, wanatoa zawadi za kila siku ikiwemo Sh 50,000 mpaka 100,000 na Sh 1 Milioni moja kila wiki.
“Katika kipindi cha miezi mitatu wakati kampeni hiyo ikiwa inaendelea, tutapata mshindi ambaye ataweza kujishindia gari lenye thamani ya Sh 23 milioni.,” alisema.
Kwenye suala zima la usalama, Madata alisema wanashirikiana kwa ukaribu mkubwa na serikali huku akiwasihi wateja wa mtandao wa Tigo kujisajili kwa alama za vidole.
Katika hatua nyingine, Afisa Huduma za Ziada, Fabian  Felician, alielezea kwamba msimu huu Tigo imeamua kushirikisha wateja wake wote kwa kuandaa maswali rahisi hususan yanayowahusu wasanii wa ndani.
“Lengo la kufanya hivi ni kudhihirisha umuhimu na mchango wa wateja wetu na pia kutambua aina ya huduma tunazozitoa,” alisema Felician

Mathalan, Meneja wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Daniel Mainoya alisema promosheni hiyo inaenda sambamba na msimu wenyewe ambao ni Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako, kwa maana ya wasanii na burudani.
Tigo Fiesta itafungua pazia mkoa wa Mwanza, Septemba 28,2019  katika viwanja vya CCM Kirumba.
Mwisho……..






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527