Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya anaedaiwa kumuua Mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa

Upande wa Jamhuri leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umesema upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe, Naomi Marijani, upo katika hatua za mwisho kukamilika.
 

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amemweleza Hakimu Mkazi, Salum Ally, kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua nzuri na za mwisho kukamilika..

Wakili Wankyo ameomba shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine ambapo kesi imeahirishwa hadi Oktoba 7, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshitakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ambapo anadaiwa kumuua Mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments