TANZANIA YAINGIA MKATABA WA UNUNUZI WA NDEGE MBILI AINA YA AIRBUS A220-300

Serikali imesaini mkataba wa ununuzi wa ndege mbili aina ya Airbus A220-300 kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL).


Mkataba huo umesainiwa leo Alhamisi Septemba 19, 2019 ambapo serikali imewakilishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Benjamin Ndimila. Airbus imewakilishwa na Makamu wa rais wa kampuni hiyo Afrika, Hadi Akoum.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Ndimila ambaye hakutaja gharama halisi inayotumika kununua ndege hizo amesema ndege hizo zitakuwa na tofauti na za aina hiyo ambayo tayari zinatumiwa na ATCL kwani kila kiti kitakuwa na 'skrini' ".

Kwa upande wake, Akoum amesema uchongaji wa ndege ya aina hiyo unachukua mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu na kwa sasa kuna oda nyingi lakini ndani ya kipindi hicho anatumaini itakuwa imekamilisha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post